Aliyepaki bajaji barabarani na kulala atiwa mbaroni

MOROGORO: JESHI la Polisi mkoani Morogoro linamshikilia dereva bajaji aliyefahamika kwa jina la Ahmaded Kipozi ,39, kwa kosa la kupaki usafiri huo barabarani na kusababisha foleni.

Katika taarifa iliyotolewa leo Jumanne Februari 11, 2025 na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, imeeleza kuwa dereva huyo alikuwa amelewa na pia hakuwa na leseni.

“Kikosi cha Usalama Barabarani kimemkamata Ahmeaded Kipozi mkazi wa Morogoro katika Barabara ya Morogoro – Dar es Salaam akiwa anaendesha bajaji bila leseni huku akiwa katika hali ya ulevi”

Advertisement

“Mtu huyo alibainika baada ya kukamatwa akiwa ameegesha bajaji hiyo Katikati ya Barabara na kusinzia kwa kuzidiwa na ulevi hivyo kusababisha foleni ndefu ambayo ilileta kero na taharuki kwa watumiaji wengine wa Barabara, Alipimwa na kupatikana na ulevi kipimo 246.2mg/100,” amesema.

Aidha, jeshi hilo limesema taratibu za kisheria za kufikishwa mahakamani kwa dereva huyo zinaendelea.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *