“Amani ni kwa wote, hata wasiokuwa na vyama”

ARUSHA: Kuhani ambaye pia ni Askofu wa Makanisa ya Kilokole ya The Pool of Shiloam Church nchini, Amani Upendo Furaha amesema kuwa unapozungumza kuhusu amani inawahusu watu wote hata kama hawana dini au hawako katika vyama vya siasa bado wanahitaji amani katika maisha yao ya kila siku.

Kuhani Furaha alisema hayo katika ibada maalumu ya kuliombea taifa juu ya waumini wa dini hiyo umuhimu wa uwepo wa amani nchini na ushiriki wa wao kupiga kura Oktoba 29 mwaka huu wa kumchagua Rais, wabunge na madiwani ibada iliyofanyika makao makuu ya kanisa hilo Kata ya Sombetini Arusha.

Alisema kila mmoja anawajibu wa kuilinda amani na kuwakemea wale wote wenye nia ovu ya kuivunja amani ya nchi kwani sio mila na destuli iliyoachwa na waasisi wa nchi hii.

Kuhani alisema kuwa kukosa haki isiwe msingi wa kukosa amani na kamwe waumini wasitumia kukosa haki kiwe chanzo cha mifarakano ya wenye kwa wenyewe.

Alisema unaweza kudai vitu vyote kama vile barabara za lami, maji, hospital, katiba mpya, mishara mikubwa lakini kukiwa hakuna amani huwezi kuvitumia vitu vyote hivyo kwa kuwa watu watasambatika huko na kule kwa machafuko ya vita hivyo aliwaasa waumini kuacha kuingia katika mtego huo wenye nia mbaya kwa taifa.

Kuhani Furaha alisema kuwa katika taifa watu hawawezi kulingana katika maamuzi na utashi wa kuchambua na kuamua mwelekeo wa jambo furani kwani kila mmoja ana maamuzi na utashi wake lakini uamuzi na utashi huo ndio unatakiwa utumike kujengana na kuleta maendeleo ya nchi ukizingatia kuelewana.

Aidha, Kuhani Furaha aliwahimiza waumini kwenda kupiga kura kwani kuchagua kiongozi ni jambo muhimu sana kwa kila mtanzania ana nafasi ya kutekeleza haki yake ya kikatiba na ni haki kuwa na kiongozi.

Alisema kura yako kama mtanzania ndio nguvu ya kuamua unayetaka akuongoze katika maisha, maamuzi ya nani unampa kura yako yanategemea utashi na malengo yako wewe kama mtanzania.

Maamuzi na utashi wa mtu mmoja hayawezi kuwa maamuzi ya taifa, lazima kuwe na wengi ili kufanya maamuzi ya pamoja,hivyo kura huumpa nafasi kila mwananchi kuamua anayetaka katika ngazi mbalimbali za uongozi.

Kuhani alisema nchi isiyokuwa na kiongozi ama uongozi haina maendeleo,haina dira, haina anayeilinda na kulisemea Taifa ikiwa hivyo kila mmoja atafanya anavyotaka na hilo sio taifa na halipo hapa duniani.

‘’Lazima twende tukapige kura na tuchagua kiongozi tunayemtaka awe Rais,mbunge ama diwani ili tutumize wajibu wetu kikatiba na tuache kuwasikiliza wanaotuhamashisha tusipige kura kwa kuwa wanatunyima haki ya msingi na wanapaswa kupuuzwa,”alisema Kuhani Furaha.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
    .
    HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button