Mpango ashiriki ibada kumuombea Baba wa Taifa

Makamu wa Rais Dk Philip Mpango ameungana na Viongozi, Waumini pamoja na Wananchi mbalimbali katika Ibada ya kumuombea Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Francisko wa Asizi, Mwanjelwa Mkoani Mbeya leo Oktoba 14, 2025.
Ibada hiyo imeongozwa na Akofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Mbeya Mhashamu Gervas Nyaisonga.



