Amlipa kijana Sh 50,000 amuue mumewe

MOROGORO; Malinyi. JESHI la Polisi Mkoa wa Morogoro linamshikilia Holo Jilia (45), mkazi wa Kijiji cha Kilolero B, Wilaya ya Malinyi , mkoani Morogoro kwa tuhuma za kula njama ya kukodisha kijana na kumlipa ujira wa Sh 50,000 ili akamuue mumewe aitwaye Charles Maghashi (55).
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama amesema hayo Novemba 3, 2023 , kuwa tukio hilo lilitokea Oktoba 29 mwaka huu, ambapo mwanamke huyo na kijana aliyetambuliwa kwa jina la Maela Athanas (33), wote wakazi wa Kijiji cha Kilolero B , wilayani Malinyi wanashikiliwa kwa tuhuma ya mauaji ya Maghashi.
Mkama alieleza sababu kubwa iliyodaiwa kusababisha mauaji ya Maghashi ni ugomvi wa kifamilia baina yao.
“ Kutokana na ugomvi huo …basi mwanamke huyo anadaiwa alikula njama na kufanya hili tukio la mauaji, “ amesema Kamanda na kuongeza kuwa kwa uchunguzi wao Athanas ilikuwa alipwe Sh 900,000, ambapo alitanguliziwa Sh 50,000..

Kwa mujibu wa Kamanda, mtuhumiwa Maela Athanas anadaiwa alikwenda nyumbani kwa marehemu na kumkuta amelala sebuleni kwake na kuanza kumkata sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia kifo chake.

Advertisement
2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *