Amuuwa rafiki yake kisa zamu ya kupika

MBEYA: JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia Mussa Basuka ,30, ambaye ni mchimbaji mdogo na mkazi wa Manyanya wilayani Chunya kwa tuhuma za kumuua rafiki yake Issa Mohamed ,30, kwa kumpiga ngumi kichwani wakati wakibishana kuhusu zamu ya kupika.

Taarifa ya Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, ACP Wilbert Siwa imesema kuwa tukio hilo limetokea Februari 18, 2025 katika Kitongoji cha Manyanya, wilayani Chunya huku chanzo kikisemekana kuwa ni mzozo uliozuka baina ya mtuhumiwa na marehemu wakiwa chumbani.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa marafiki hao wawili walikuwa ndani ya chumba walichokuwa wamepanga, na walikuwa wamelewa hivyo wakaanza kubishana kuhusu zamu ya kupika chakula cha jioni ambapo marehemu alikuwa na jukumu la kupika na mtuhumiwa alikuwa na jukumu la kuchota maji.

Aidha, Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi kuzingatia utulivu na sheria katika kushughulikia migogoro ili kuepusha madhara kama haya.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button