Anaswa kwa tuhuma za kumuua kiongozi wa dini

SONGWE: JESHI la Polisi mkoani Songwe limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja kwa tuhuma za mauaji ya Katekista wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu Tazara Tunduma wilayani Momba aliyefahamika kwa jina la Vincent Mwenda.

Hayo yamethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Augustino Senga wakati alipozungumza waandishi wa habari mapema leo Mei 22, 2025 mkoani hapa.

Amesema tukio la mauaji ya Katekista Vincent Mwenda (38) mkazi wa mtaa wa migombani Tunduma ambaye pia alikuwa fundi ujenzi lilifanyika Mei, 10, 2025 kwa kushambuliwa na kitu chenye ncha kali na maeneo mbalimbali ya mwili wake.

ZAIDI SOMA: Watuhumiwa 11 wa uganga wanaswa Songwe 

Kamanda Senga amemtaja mtuhumiwa aliyekamatwa kuwa anatambulika kwa jina la Lameck Meltus Mwamlima (29), fundi magari mkazi wa migombani Tunduma ambaye alikamatwa Mei, 20, 2025.

“Uchunguzi wa awali umebainisha kuwa sababu za mauaji hayo ni wivu wa kimapenzi ambapo mtuhumiwa alikuwa akimtuhumu marehemu kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mke wake,” amesema Afande Senga.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button