Watuhumiwa 11 wa uganga wanaswa Songwe

JESHI la Polisi Mkoa wa Songwe limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 11 wanaojishuhulisha na uganga bila kibali.

Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Theopista Mallya imesema katika operesheni iliyofanywa na jeshi hilo Januari 9 mwaka huu walifanikiwa kumkamata chifu wa kabila la Kinyiha aitwaye Mwene Nzunda (44) mkazi wa kijiji cha Nambala pamoja na wenzake.

AIdha aliwataja watuhumiwa wengine kama, Anthony Yatilinga Mapumba (65) mkazi wa Ilembo, Isambi Yasinta Mghallah (80) mkazi wa Majengo, Kostebo Ngawelo Mziho (53) mkazi wa Nambala, Tamimu Balison Mdollo (57) mkazi wa Ilembo, Biton Daimon Nzunda (64) Balozi mtaa wa Nsenya Shina namba 8 na mkazi wa Nsenya, Amos Nzunda (23) Steven Mwilenga (46) David Frank Mapumba (72) mkazi wa Ilembo, George Greyson Mghala (43) mkulima, mkazi wa mtaa wa Danida kijiji cha Ilembo na Jailos Sola (42) mkulima na mkazi wa Mbimba.

Advertisement

Kwa upande wa watuhumiwa hao walielewa kuwa katika kijiji hicho kuna mambo yanayofanyika yanayoashiria kuwa ni yakishirikina ambapo jeshi la polisi likaeleza kuwa linaendelea na upelelezi wa kesi ili watuhumiwa waweze kufikishwa mahakamani.

Jeshi hilo ilitoa onyo vikali kwa wanaoendesha shughuli za kignaga bila kibali likisema ni marufuku kwa mtu yoyote kufanya shughuli za uganga bila kibali ikiwa ni pamoja na kitendo cha kusafisha nyumba zinazodhaniwa kuwa na uchawi kwani kitendo hicho kinaleta chuki na udhalilishaji kwa jamii.