Angalizo lizingatiwe ajira kwa watendaji vituo vya uchaguzi

TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) inaendelea kufanya mafunzo kwa watendaji wa Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Mafunzo hayo yanajumuisha waratibu wa uchaguzi, wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo.
Inec imegawa mafunzo hayo kwenye awamu mbili na hii ni ya kwanza ikihusisha watendaji kutoka mikoa ya Morogoro, Singida, Dodoma, Kaskazini Unguja, Kusini Unguja, Mjini Magharibi, Geita, Kagera, Mtwara, Lindi, Tabora, Kigoma, Tanga, Kilimanjaro, Ruvuma, Iringa na Njombe.
Tume kupitia viongozi wake, wamekaririwa wakitoa nasaha mbalimbali kwa watendaji hao huku nyingi zikijielekeza kuwataka wawe chachu ya uchaguzi unaozingatia katiba, sheria, kanuni, miongozo na maelekezo yanayotolewa na yatakayotolewa na Inec.
Mathalani, Mwenyekiti wa INEC, Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jacobs Mwambegele amewataka wajiepushe kuwa vyanzo vya malalamiko kutoka kwa vyama vya siasa na wadau wa uchaguzi.
Jambo lingine alilotoa ni wito kuhusu ajira za watendaji wa vituo akisisitiza kwamba zizingatie kuajiri wenye weledi, wanaojitambua, wazalendo, waadilifu na wachapakazi na kuachana na upendeleo kwa ndugu na jamaa ambao hawana sifa za kufanya shughuli za uchaguzi.
Tunapongeza na kuunga mkono angalizo hili la Jaji Mwambegele kwa kuzingatia athari za kutozingatia weledi katika kuajiri watu wa kufanya kazi hii nyeti ya masuala ya uchaguzi.
Siku zote, penye upendeleo huwa hapaangalii matokeo yenye tija bali ni kwa masilahi binafsi. Upendeleo unaweza kuingiza watu wasioelewa na matokeo yake, wakawa chanzo cha uchaguzi kuchezewa na hivyo kupunguza imani ya wananchi kwenye matokeo.
Inawezekana kabisa wakaajiriwa watu wasio na maadili, uwezo, uzalendo au watu wenye ‘ajenda’ zao na matokeo yake wakatia doa mchakato huu muhimu kwa ustawi wa taifa.
Endapo ajira zitazingatia upendeleo wa undugu, ukabila, rangi na vigezo vinginevyo, ni rahisi kuingiza hata watu wasiostahili wakiwamo ambao wamekuwa wakinyooshewa kidole kutokana na maadili na uadilifu wao kuwa wenye shaka.
Matokeo yanayoweza kujitokeza ni pamoja na kushuka kwa imani ya wananchi kwenye taasisi za uchaguzi, kuzidisha migogoro ya kijamii na kuleta hali ya uvunjifu wa amani. Hii inaweza kuathiri usalama wa taifa na maendeleo ya nchi kwa ujumla.
Ndiyo maana tunasema rai ya Jaji Mwambegele ni muafaka na muhimu kuzingatiwa na mamlaka husika kwa kuhakikisha ajira za watendaji haziangalii ndugu na jamaa ambao hawana sifa za kufanya shughuli za uchaguzi.
Kwa muktadha huo, ikitokea wakaajiriwa watu wasiofaa na ikabainika waliofanya hivyo waliongozwa na misingi ya upendeleo, mamlaka zinazohusika zisisite kuchukua hatua stahiki.
I get paid over $130 1 to 3 hours working from home with 2 kids at home. I never thought I’d be able to do it but my best friend earns over $27k a month doing this and she convinced me to try. The potential with this is endless.
Heress———–> http://www.now.jobs67.com
Getting paid Every month more than $25,000 by doing very simple Online job from home.i m doing this job in my part time i have earned and received $25861 last month .I am now a good Online earner and earns enough cash for my needs. Every person can get this Online job.follow details on this website…
Go Here——➤ http://www.get.money63.com
Getting paid Every month more than $25,000 by doing very simple Online job from home.i m doing this job in my part time i have earned and received $25861 last month .I am now a good Online earner and earns enough cash for my needs. Every person can get this Online job.follow details on this website…
Go Here——➤ http://www.get.money63.com