Araqchi: Tupo tayari tukiona nia njema

TEHRAN: WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araqchi, amesema nchi yake iko tayari kurejea kwenye mazungumzo ya mkataba wa nyuklia endapo mataifa ya Magharibi yataonyesha nia njema.

Katika barua aliyomwandikia Mkuu wa Sera za Mambo ya Nje wa Umoja wa Ulaya, Kaja Kallas, Araqchi alisisitiza utayari wa Iran kuanza tena mazungumzo ya kidiplomasia kwa haki na usawa ili kuepuka vitendo vinavyoweza kuhatarisha uwezekano wa kufikiwa kwa makubaliano mapya.

Araqchi alitoa kauli hiyo saa chache baada ya Uingereza, Ufaransa na Ujerumani kuanzisha mchakato wa siku 30 wa kuiwekea Iran vikwazo vipya vya Umoja wa Mataifa kufuatia mpango wake wa nyuklia.

Wakati huo huo, Umoja wa Mataifa umezitaka Iran na mataifa hayo matatu ya Ulaya kuongeza kasi ya mazungumzo ili kufikia makubaliano ndani ya siku 30 zijazo, kabla ya kurejeshwa kwa vikwazo hivyo vilivyochochewa na hatua za Ulaya. SOMA: Mazungumzo ya nyuklia Iran yapwaya

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button