Argentina yaanza vyema kutetea taji la Copa America

ATLANTA: BINGWA mtetezi wa Kombe la Copa America, Argentina imeanza vyema kutetea taji hilo baada ya kuibuka na ushindi mabao 2-0 dhidi ya Canada katika mechi ya ufunguzi wa michuano hiyo hatua ya makundi.
Argentina inasaka taji lake la tatu mfululizo baada ya kushinda Copa America ya 2021 na Kombe la Dunia la 2022 na imeanza kampeni hiyo kundi A katika uwanja wa Mercedes-Benz uliopo Atlanta, Georgia Marekani.
Messi, ambaye atafikisha miaka 37 Juni 24, alitengeneza bao la kwanza alipopitisha pasi katikati ya walinzi wa Canada kwenda kwa Alexis Mac Allister aliyeupiga mpira kwa mguu wa kulia na Julián Álvarez kufunga dakia 49 huku akigongana na mlinda lango Maxime Crépeau.
Kisha Messi akatoa pasi ya bao la pili la Lautaro Martínez dakika ya 88.
Messi amevunja rekodi ya Copa America kwa kucheza mechi yake ya 35, moja zaidi ya Sergio Livingstone wa Chile kuanzia mwaka 1941 hadi 1953. Messi ameendeleza rekodi yake mwenyewe kwa kutoa pasi ya 18.
Kipute cha mashindano hayo leo ni kati ya Peru na Chile katika uwanja wa AT&T uliopo Arlington, Texas.
Michuano ya Copa America 2024 inafanyika Marekani ambapo timu mbili za kwanza za makundi zitafuzu robo fainali.
Robo fainali zitaanza Julai 5. Michezo ya nusu fainali itachezwa Julai 9 na 10 ikifuatiwa na fainali Julai 14.
Makundi ya michuano ya Copa America 2024 ni kama ifuatavyo:
KUNDI A
Argentina
Peru
Chile
Canada
KUNDI B
Mexico
Ecuador
Venezuala
Jamaica
KUNDI C
Marekani
Uruguay
Panama
Bolivia
KUNDI D
Brazil
Colombia
Paraguay
Costa Rica

Habari Zifananazo

Back to top button