Arsenal, Kavertz mambo yaanza kunoga

UWEZEKANO wa Arsenal kuinasa saini ya kiungo Kai Havertz kutoka kwa mahasimu wao Chelsea unazidi kuwapa matumaini baada ya makubaliano binafsi kuafikiwa kati ya pande hizo mbili.
Taarifa ya mwandishi wa habari za michezo, Fabrizio Romano imeeleza Havertz hataki kuendelea kubaki Chelsea, huku Arsenal ikiwa klabu pekee inayoongoza mashambulizi ya kumsajili.
Romano amesema Chelsea wanataka pauni milioni 75, Arsenal hawapo tayari kulipa kiasi hicho cha pesa.
Bayern Munchen imetaarifiwa juu ya upatikanaji wa Mjerumani huyo ila bado wako kimya, Real Madrid imejiondoka kwenye mbio za kumsajili.