Arsenal kuvaana na Sheffield leo
LIGI Kuu England inaendelea leo ambapo Arsenal watafunga raundi ya 27 watakapokuwa wageni wa Sheffield United uwanja wa Bramall Lane, mchezo huo utapigwa saa 5:00 usiku.
Arsenal ikiwa kwenye nafasi ya tatu katika msimamo wa EPL, imeshakusanya pointi 58, huku wakihitaji kushinda mchezo huo ili kuendelea kupunguza pengo la pointi nne na tano dhidi ya Man City na Liverpool baada ya kushinda mechi zao wikiendi.
Sheffield inashika nafasi ya mwisho 20, wakiwa na pointi 13, baada ya kucheza michezo 26. Wameshinda mechi tatu, sare nne wamefungwa 19.
Taarifa njema kwa Arsenal ni kurejea kwa Thomas Partey ambaye alikuwa majeruhi kwa muda mrefu, Gabriel Jesus, Takehiro Tomiyasu, Alexander Zinchenko ambao woye wamerejea. Pia Jullien Timber amerejea ingawa anaweza asiwe sehemu ya kikosi cha leo.



