Arsenal yafuzu nusu fainali UEFA kwa mara ya tatu

SPAIN — Klabu ya Arsenal imeandika historia tena baada ya kufuzu nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya tatu katika historia yake.

Hii ni baada ya kuifunga Real Madrid mabao 2-1 katika mechi ya marudiano iliyopigwa jana usiku kwenye Uwanja wa Santiago Bernabéu, na kumaliza na jumla ya mabao 5-1.

Bukayo Saka na Gabriel Martinelli waliifungia Arsenal huku Vinícius Júnior akiipatia Real bao la kufutia machozi. Ushindi huu unaendeleza rekodi bora ya vijana wa Mikel Arteta msimu huu barani Ulaya, na sasa watakutana na Paris Saint-Germain kwenye hatua ya nusu fainali.

Arsenal ilifika nusu fainali mara ya kwanza mwaka 2006, kisha ikarudia tena mwaka 2009.

Mwaka huu 2025, The Gunners wanarejea katika hatua hiyo wakiwa na matumaini makubwa ya kutinga fainali na kuandika historia mpya ya kutwaa taji lao la kwanza la UEFA Champions League.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button