Arusha yazindua mitambo kutengeneza barabara korofi

HALMASHAURI ya Jiji la Arusha imezindua mitambo mipya ya kutengeneza barabara korofi za jiji hilo ikiwemo malori mawili yaliyonunuliwa kwa fedha za mapato ya ndani zaidi ya Sh bilioni 2.

Akizungumza leo mkoani kwenye halfa ya uzinduzi wa mitambo hiyo, Meya wa Arusha, Maximilian Iraqhe amewaomba madiwani kushirikiana na wananchi kuainisha barabara wanazohitaji kutengenezwa.
“Vifaa hivi vimenunuliwa na fedha za mapato ya ndani ambazo kimsingi ni fedha za wananchi, hivyo muhimu mitambo hii itunzwe idumu zaidi ya miaka kumi,”alisema.

Amesema mashine hizo zitaanza kazi kuanzia kesho kwenye kata kubwa ya Kata ya Olorien, Kata ya Murieti, Moshono na Olasiti na baada ya hapo katika kata zingine.
Amesema mtambo na malori hayo yataanza kazi katika barabara zisizo na vigezo vya kutengezwa na Wakala wa Barabara vijijini na mijini (TARURA) ambao wanahitaji barabara yenye upana wa mita 12.
“Hizi barabara za mitaani zenye pungufu ya mita hizo 12 tutatengeneza na mitambo ya jiji na kazi hii inaanza mara moja,”



