Asilimia 15 Watanzania wanaishi na vinasaba selimundu

DODOMA; SERIKALI imesema Tanzania ni miongoni mwa nchi tano duniani zinazoongoza kwa idadi kubwa ya ugonjwa wa selimundu, ambapo asilimia 15 ya watanzania wanaishi na vinasaba vya ugonjwa huo.

Kauli hiyo imetolewa bungeni mjini Dodoma leo na Waziri wa Afya, Jenista Mhagama alipokuwa hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya Wizara ya Afya kwa mwaka 2025/2026.

“Katika kudhibiti ugonjwa huu, wizara kwa kushirikiana na wadau imeanzisha kampeni maalum ya elimu ya ugonjwa wa selimundu na kampeni ya vunja mduara ambayo inalenga vijana kutambua hali zao ya vinasaba.

“Katika kipindi cha Julai 2024 hadi Machi 2025, jumla ya vijana 10,601 kutoka mikoa ya Mwanza, Morogoro, Pwani, Mara, Arusha, Dodoma, Dar es Salaam na Tabora walipatiwa elimu na fursa ya kupima vinasaba vya ugonjwa wa Selimundu.

“Aidha, Wizara pia ilitoa elimu ya ugonjwa adimu wa Himofilia kwa wazazi, walezi na wagonjwa 1,690 katika Mikoa ya Morogoro, Manyara, Tanga na Arusha,” amesema Waziri Mhagama.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button