Askari 23 kuhukumiwa kifo kwa kusaliti jeshi

DR CONGO : ZAIDI ya wanajeshi Ishirini wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanakabiliwa na adhabu ya kifo au vifungo vya miaka 10 hadi 20 jela.
Kwa mujibu wa Msemaji wa jeshi la Kongo Luteni Kanali MaK Hazukay amesema askari hao walifikishwa mbele ya mahakama ya kijeshi mjini Butembo katika mkoa wa Kivu Kaskazini.
Vikosi vya usalama kwa miaka mingi vimekuwa vikipambana na zaidi ya makundi 120 ya waasi katika eneo la mashariki mwa Kongo lenye utajiri mkubwa wa rasilimali za madini.
Kongo iliondoa marufuku iliyodumu kwa miaka 20 ya adhabu ya kifo mwezi Machi, hatua iliyokosolewa na wanaharakati wa haki za binaadamu.
Hatahivyo, mwezi mei mwaka huu askari wanane walihukumiwa adhabu ya kifo kwa kutoroka mapigano na mwezi julai wengine 25 walihukumiwa kwa makosa kama hayo.
Hadi sasa bado haijaweza kubainisha kama kuna askari wowote walionyongwa kufuatia muongozo wa adhabu hii. SOMA: Hatma DR Congo Rwanda haijulikani



