Askari sita mbaroni kwa mauaji

DAR ES SALAAM: JESHI la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam amethibitisha kukamatwa kwa maaskari sita wa jeshi la polisi, walinzi 11 wa kampuni ya ulinzi ya Pasco Ltd, na maafisa misitu wa (TFS) wawili.

Kamanda Kanda Maalum ya Dar es Salaam,  Muliro Jumanne (SACP) amesema kushikiliwa kwa watu hao kunatokana na tuhuma za kujeruhiwa kwa watu wawili ambao baadae walipoteza maisha na suala hilo uchunguzi wake tayari unaendelea kufanyika.

“Agosti 28 Agosti, 2023 majira ya saa nane  usiku eneo la Kiluvya Ubungo, maafisa kutoka katika taasisi hizo wanadai wakati wa utekelezaji wa majukumu yao, lilitokea kundi la watu wanaokadiriwa kuwa 30 wakiwa na pikipiki zilizokuwa zimebeba magunia ya mkaa.”Amesema na kuongeza

“Mkaa ni mazao ya misitu na walipofika eneo la ukaguzi na kuamriwa wasimame, walikaidi na kuanza kufanya fujo kubwa kwa kuwarushia mawe Maofisa wa maliasili na wenzao wakishinikiza pikipiki zilizo kuwa na mkaa kinyume na sheria ziachiwe.”Amesema Muliro

Amesema, Mafisa wa timu hiyo waliokuwa na silaha walianza kufyatua risasi kwa lengo la kuwatawanya na kujilinda.

“Hata hivyo ilibainika watu wawili walijeruhiwa katika purukushani hizo na walipoteza maisha baada ya kufikishwa hospitali ya Mloganzila.”Amesema

Amesema, katika tukio hilo Pikipiki 16 ambazo zilitelekezwa na watu hao na magunia ya mkaa vilipelekwa Mpingo House.

“Jeshi la Polisi Kanda Maalum linachunguza mazingira yote ya tukio hili kwa kushirikiana na mamlaka zingine za kisheria na halitasita kuwezesha kuchukuliwa kwa hatua zingine za kisheria kulingana na sheria za nchi.

Amesema, watu waliokuwa kwenye kazi hiyo wako chini ya ulinzi na silaha zao zimepelekwa kwenye mamlaka za kiuchunguzi za silaha/bunduki na miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Mloganzila kwa uchunguzi

Habari Zifananazo

7 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button