Askari watoa msaada kituo cha watoto yatima.

Askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha waliotimiza 22 kazini, wametoa msaada katika kituo cha kulea watoto yatima cha ‘faraja Orphanage’ kilichopo shangalai Wilaya ya Arumeru ikiwa ni mchango wao kwa kituo hicho.

Akizungumza kwa niaba ya askari wenzake Sajenti Mwanema amesema wameona ni vyema kutoa msaada huo ambao umeenda sambamba na shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwa kuwalinda kipindi cha miaka ishirini na mbili kazini.

Amesema kuwa imekuwa ni utamadunia wa askari Polisi kutoa msaada kwa makundi yenye uhitaji ambapo amewaomba watu wengine kutoa walicho nacho kwa watoto wenye uhitaji katika vituo vya watoto yatima.

Mkurungenzi wa kituo hicho, Mchungaji Faraja Malaki amewashukuru askari hao kwa mchango na msaada wao katika kituo hicho na kuwaomba wengine wenye moyo wa kujitoa wafike kituo cha faraja kusaidia watoto hao wenye uhitaji.

Jephason Faraja ambaye ameongea kwa niaba ya watoto wenzake wanaolelewa katika kituo hicho amewashukuru askari hao kwa kutoa msaada huo ambao umefanya wajisikie ni kundi linalokumbukwa katika Jamii.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button