ATCL kuanza safari Ulaya na Asia

TANGA: Kampuni ya ndege Tanzania ATCL inatarajia kuongeza masafa Kwa kuanza safari za ndege kwenye bara la Asia na Ulaya ikiwemo kuongeza masafa Kwa baadhi ya mikoa hapa nchini.

Hayo yamesemwa na Mkurungenzi Mtendaji wa shirika hilo Mhandisi Ladslaus Matindi wakati wa hafla ya kugawa vifaa katika shule ya sekondari ya Tanga Ufundi .

Amesema kuwa wanatarajia kuanza safari za India na China hivi karibuni pamoja na bara la ulaya ili kufungua milango ya fursa za kiuchumi katika maeneo hayo .

“Hivi karibuni tunaanza safari za ndege kati ya Tanga, Pemba na Musoma mara baada ya maboresho yanayoendelea yatakapo kamilika”amesema Mhandisi Matindi.

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba amewataka wanafunzi wa kike kuchangamkia fursa ya masomo ya sayansi na uhandisi ili kuongeza uwiano wa marubani wa ndege wanawake nchini.

ATCL imetoa msaada wa meza na viti vyenye thamani ya Sh miionil 70 Kwa ajili ya kutumiwa na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Tanga Ufundi katika bwalo la chakula.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button