ATCL kuongeza vituo vitatu kimkakati

SERIKALI imesema Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) linazidi kuimarika na litaongeza vituo vitatu kimkakati. Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa alisema hayo Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari jana.

“Tuna ndege 16 sasa hivi, na wote mmesikia wakati wa kampeni maana yake sasa hivi tunaanza kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi, tunakwenda kuongeza ndege zingine nane shirika letu lifikishe ndege 24,” alisema Msigwa. Amesema serikali inaongeza vituo vitatu vya kimkakati vya ndege mbali ya 29 vya nje na ndani ambavyo ATCL inatoa huduma kwa sasa.

“Mpaka mwisho wa mwaka huu tutaongeza Cape Town, Afrika Kusini, mnajua tunakwenda Johannesburg tayari, tunaongeza Accra, Ghana na tunaongeza Victoria Falls kule Zimbabwe,” alisema Msigwa. SOMA: ATCL inavyofungua uchumi Pemba

Amesema vituo hivyo vya kimkakati ni kutokana na safari za watalii wanaotembelea Tanzania, wengi wakitoka kwenye vivutio vya Tanzania husafiri kuelekea kwenye hiyo miji aliyoitaja. “Tumeshaona watalii wakishatembelea Tanzania wanakwenda Victoria Falls na wakishatembelea Victoria falls wanataka kwenda kwenye vivutio vingine, tunaweka ndege itakwenda kule itapeleka watalii kule na italeta watalii Tanzania.

Tutaongeza idadi lengo letu ikifika mwaka 2030 tufikie vituo 50 vya ndani na nje ya nchi,” alisema Msigwa. Amesema ATCL kwa sasa inahudumia abiria 1,500,000 lakini lengo ni kufikia abiria milioni tatu katika miaka miwili ijayo. “Hapa tumepiga hatua tulikuwa kama laki nane, tumefika milioni moja na nusu, tunakwenda kwenye milioni tatu miaka miwili ijayo,” alisema Msigwa.

Msigwa amesema sekta ya utalii nchini imeimarika kiasi cha kuvuka lengo lililowekwa na serikali katika mwaka 2024 hadi 2025. “Kwenye utalii huko ndio usiseme, wote mnafahamu, tulikuwa tumeweka lengo la kupokea watalii milioni tano ifikapo mwaka 2025. Tumemaliza mwaka 2024 tumefikisha watalii milioni 5.3, mpaka mwisho wa mwaka huu tutawapa takwimu zingine lakini idadi ya watalii imeongezeka sana,” alisema.

Amesema awali Tanzania ilikuwa inapokea watalii kati ya milioni mbili hadi milioni moja na kitu, wakati mwingine ilipokea watalii 700,000 lakini mambo yakienda vizuri nchi itapokea watalii milioni nane ifikapo mwaka 2030. Msigwa amesema utalii unapoongezeka ni neema kwani ni sehemu ya kukuza uchumi na kuchochea maendeleo ya nchi.

Amesisitiza Watanzania kutoshiriki katika matukio ya uvunjifu wa amani yatakayoifanya sekta hiyo kutetereka. “Watalii tunapozungumzia milioni nane ndio haohao waliokuwa wanakwenda kwa washindani wetu katika utalii, sasa watakuja Tanzania, kule wanakohama watafurahi?” alisema.

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. How can we Transform “Dreams to Death” – I have something to say about you (you will get through dreams

    1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
      .
      This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

    2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
      .
      M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button