Ateba ruksa kucheza ligi kuu

DAR ES SALAAM: MSHAMBULIAJI mpya wa Simba, Leonel Ateba ruska kuitumikia klabu hiyo katika michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kukamilika vibali vya kazi pamoja na ITS yake kuwasili.

Nyota huyo huenda akawa katika kikosi cha Simba katika mchezo ujao dhidi ya Fountain Gate FC utakaochezwa Jumapili, Agosti 25, 2024, uwanja wa KMC, uliopo Mwenge, Dar es Salaam.

Ateba ni usajili wa kocha mkuu wa Simba Fadlu Davids akiutaka uongozi wa timu hiyo kuongeza mshambuliaji na kuchukuwa nafasi ya Freddy Michael ambaye tayari ameagwa.

Meneja wa idara ya habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema wamekamilisha taratibu zote za vibali vya mshambuliaji wao Ateba na sasa rasmi kucheza mechi.

Amesema mechi ya Tabora United alishindwa kucheza baada ya vibali vyake kutokamilika ikiwemo ITS kutoka klabu USM Alger, tayari imewasili na ruksa nyota huyo mechi zijazo.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Simba Sports Club (@simbasctanzania)

“Tumekamilisha taratibu zote za vibali, Ateba sasa ruksa kucheza ligi, hata tukipangiwa mechi leo mshambuliaji huyo yupo tayari kucheza, ni mipango ya kocha Fadlu tu kumtumia,” amesema Ahmed.

SOMA: Ateba aja na moto ligi kuu

Ameongeza kuwa timu hiyo inaendelea na maandalizi, pamoja na kushinda dhidi ya Tabora United, wanahitaji kuwapa muda zaidi wachezaji wao waendelee kutafuta ubora wao.

“Tumesajili Wachezaji bora sana wamefanya makubwa walikotoka, katika hao Wapo walioanzia juu moja kwa moja na wengine wameanzia chini, iko hivyo duniani kote hasa Mchezaji anapotoka timu ndogo kwenda kubwa au kutoka ligi ndogo kwenda kubwa au anapoenda kwenye timu yenye presha kubwa kama yetu

Ni jukumu letu kuwavumilia, kuwatia moyo, kusimama nao nyakati zote ili warejeshe kujiamini na kuupata ubora wao,aina ya Wachezaji tuliokua nao nusu yao wakiupata ubora wao basi Mwaka huu utakua Msimu mzuri kwetu,” amesema Ahmed.

Habari Zifananazo

Back to top button