Athari zuio usafirishaji vipepeo latua bungeni

DODOMA; MBUNGE wa Donge, Mohamed Jumah Soud, amehoji bungeni mpango wa serikali kukaa na sekta inayohusika na biashara ya vipepeo upande wa Zanzibar, kwani wafanyabiashara hiyo wameathirika na zuio la usafirishaji wanyama hai nje ya nchi.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Dunstan Kitandula, amesema Serikali iliweka zuio la biashara ya ukamataji na usafirishaji wa wanyamapori hai nje ya nchi kutokana na dosari kadhaa zilizokuwa zimejitokeza katika uendeshaji wa biashara hiyo.

‘’Kufuatia zuio hilo, Serikali iliunda Kamati ya Wataalam kwa ajili ya kufanya tathmini ya zuio na kuwasilisha mapendekezo kuhusu mustakabali wa biashara hii.

‘’Kamati hiyo ilipokea maoni na mapendekezo kutoka pande zote mbili za Muungano kwa kuwa masuala ya wanyamapori yanasimamiwa kwa sheria mbili tofauti kwa Bara na Visiwani.

‘’Mheshimiwa Spika, suala la biashara ya vipepeo ni miongoni mwa masuala yaliyojadiliwa katika vikao rasmi vya mashirikiano kati ya Wizara ya Maliasili na Utalii na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi ya Zanzibar. Kwa sasa Wataalam wanakamilisha taarifa na mapendekezo, ili yaweze kuwa msingi wa kufanya maamuzi ya mustakabali wa biashara hiyo,” amesema Naibu Waziri.

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button