Atoa maagizo vituo uwezeshaji wananchi kiuchumi

DAR ES SALAAM; Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), ACP Beng’i Issa, ametembelea vituo vitatu vya uwezeshaji wananchi kiuchumi jijini Dar es Salaam na kutoa maagizo mbalimbali yenye lengo la kuboresha utoaji wa huduma na kuongeza mchango wa vituo hivyo kukuza uchumi wa Taifa.
ACP Issa alitembelea kituo cha Innovate Hub, ambacho kinajishughulisha na kulea, kuwaendeleza na kuwaunganisha wajasiriamali na wawekezaji, ili waweze kupata mitaji na fursa za biashara.

Akiwa kituoni hapo, alisisitiza umuhimu wa kuongeza ushirikiano kati ya wajasiriamali, taasisi za fedha na sekta binafsi ili kukuza ubunifu na biashara zinazoweza kutoa ajira kwa vijana.
Pia alitembelea kituo cha CoICT – Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), ambacho hutoa mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) pamoja na kuendeleza programu bunifu zinazolenga kutatua changamoto mbalimbali za kijamii na kiuchumi kupitia matumizi ya teknolojia.

Aliipongeza CoICT kwa mchango wake katika kukuza uchumi wa kidijitali na kuwataka waendelee kuandaa vijana kuwa wabunifu na wajasiriamali wa teknolojia.
Ziara hiyo ilihitimishwa katika Kituo cha Uwezeshaji, ambacho kina vitengo mbalimbali vinavyotoa huduma kwa wananchi, ikiwemo utoaji wa mikopo, ushauri wa kibiashara na mafunzo kwa wajasiriamali ili kuwawezesha kuanzisha na kukuza biashara zao.
Akiwa hapo, alitoa maagizo ya kuboreshwa kwa mifumo ya utoaji huduma ili iwe rahisi zaidi kwa wananchi kupata taarifa, mikopo na msaada wa kitaalamu




l Get paid over $110 per hour working from home. l never thought I’d be able to do it but my buddy makes over $21269 a month doing this and she convinced me to try. The possibility with this is endless….
This is what I do………………………………….. https://Www.Cash54.Com
I am making a real GOOD MONEY (300$ to 400$ / hr )online from my laptop. Last month I GOT check of nearly 18,000$, this online work is simple and straightforward, don’t have to go OFFICE, Its home online job. At that point this work opportunity is for you.if you interested.simply give it a shot on the accompanying site….Simply go to the BELOW SITE and start your work…
This is what I do………………………………….. https://Www.Payathome9.Com