Atupwa jela miaka 30 kwa kumlawiti mgonjwa wa akili

TABORA; MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Nzega mkoani Tabora, imemhukumu mkulima na mkazi wa Kata ya Mbagwa wilayani humo, Boniface Matale (30) kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti kijana mwenzake mwenye matatizo ya akili.
Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu mkazi mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Nzega, Nasra Mkadam na kusema ametoa hukumu hiyo ili iwe fundisho kwa watu wengine.
Alisema mahakama imeridhika na ushahidi uliotolewa mbele ya mahakama hiyo na usiotia shaka yoyote, hivyo imeridhia Boniface Matale aitumikie adhabu ya miaka 30 jela.
Hakimu Nasra alisema adhabu hiyo itakuwa fundisho kwake na watu wengine wenye nia ya kufanya vitendo hivyo vya kikatili kwa watu wenye matatizo ya akili kama kijana huyo.
Nasra aliendelea kuiambia mahakama hiyo kwa kusema kwamba vitendo vya ukatili vya ubakaji na ulawiti vimekuwa vikitokea mara kwa mara kwenye Wilaya ya Nzega na adhabu hizo zitakuwa ni fundisho kwa wengine.
Awali, Wakili wa Serikali, Enock Kigolya aliieleza mahakama hiyo kwamba Agosti 19, 2025 majira ya usiku katika Kata ya Mbagwa nyumbani kwa kijana huyo, Matale aliingia na kumlawiti.
Alisema kitendo hicho kilishuhudiwa na dada wa kijana huyo mwenye matatizo ya akili ambaye hata kuzungumza hawezi kutokana na matatizo hayo ya akili.
Mshitakiwa huyo aliomba kupunguziwa adhabu kwa kuwa ana umri mdogo na anategemewa na wazazi wake.
I am making a real GOOD MONEY (80$ to 92$ / hr. )online from my laptop. Last month I GOT a check of nearly 21,000$, this online work is simple and straightforward, I don’t have to go to the OFFICE. At that point this work opportunity is for you. If you are interested. Simply give it a shot on the accompanying site link… https://Www.EarnApp1.Com
I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
.
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com