Australia yatangaza kuitambua Palestina

CANBERRA, AUSTRALIA : SERIKALI ya Australia imetangaza kuitambua rasmi Palestina kama taifa huru katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa unaotarajiwa kufanyika Septemba mwaka huu, hatua inayofuatia maamuzi sawa ya mataifa kama Uingereza, Ufaransa na Canada.
Waziri Mkuu wa Australia, Anthony Albanese, amesema uamuzi huo umetanguliwa na makubaliano muhimu kati ya Australia na Mamlaka ya Palestina. Makubaliano hayo yanajumuisha masharti ya kupokonywa silaha kwa makundi yenye silaha, kufanyika kwa uchaguzi mkuu, na uthibitisho wa Palestina kulitambua taifa la Israel na haki yake ya kuendelea kuwepo.
“Suluhisho la mataifa mawili tofauti ndilo tumaini la kweli kuvunja mzunguko wa vurugu katika Mashariki ya Kati, na kumaliza migogoro, mateso na baa la njaa linaloikumba Gaza,” alisema Albanese.
Hata hivyo, Israel imekosoa uamuzi huo ikisema kutambuliwa kwa Palestina ni sawa na kukubali ugaidi, huku ikikabiliwa na shinikizo la kimataifa la kusitisha vita vinavyoendelea Gaza. Taarifa ya Wizara ya Afya inayoendeshwa na Hamas imesema tangu Jumamosi iliyopita watu watano wamefariki dunia kutokana na njaa na utapiamlo huko Gaza, na idadi ya vifo kufikia 217.
Aidha, tangu kuanza kwa mashambulizi ya kijeshi ya Israel mwaka 2023, zaidi ya watu 61,000 wamepoteza maisha. Mashambulizi hayo yalizuka kufuatia uvamizi mkubwa ulioongozwa na kundi la Hamas Oktoba 7, 2023, ambapo watu wapatao 1,200 waliuawa na wengine 251 kuchukuliwa mateka.
Kwa upande wake, Mamlaka ya Palestina inayosimamia baadhi ya maeneo ya Ukingo wa Magharibi imesema hatua hiyo ni ishara ya kuongezeka kwa uungwaji mkono wa kimataifa kwa haki ya Wapalestina ya kujitawala.
Waziri Mkuu Albanese alieleza kuwa uamuzi wa serikali yake umetokana na ahadi ya Rais wa Mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas, kuwa Hamas haitakuwa na nafasi katika uongozi wa taifa la Palestina litakapoundwa. Hatua hiyo pia ni matokeo ya mashauriano ya karibu kati ya Australia na viongozi wa mataifa mengine, yakiwemo Uingereza, Ufaransa, New Zealand na Japan, yaliyofanyika katika kipindi cha wiki mbili zilizopita.
“Tunaamini huu ni wakati wa fursa ya kihistoria, na Australia iko tayari kushirikiana na jumuiya ya kimataifa kuitumia ipasavyo,” alisema Albanese. SOMA: Canada kuunga mkono Palestina
Waziri Mkuu wa Australia, Anthony Albanese, amesema uamuzi huo umetanguliwa na makubaliano muhimu kati ya Australia na Mamlaka ya Palestina. Makubaliano hayo yanajumuisha masharti ya kupokonywa silaha kwa makundi yenye silaha, kufanyika kwa uchaguzi mkuu, na uthibitisho wa Palestina kulitambua taifa la Israel na haki yake ya kuendelea kuwepo.
“Suluhisho la mataifa mawili tofauti ndilo tumaini la kweli kuvunja mzunguko wa vurugu katika Mashariki ya Kati, na kumaliza migogoro, mateso na baa la njaa linaloikumba Gaza,” alisema Albanese.
Hata hivyo, Israel imekosoa uamuzi huo ikisema kutambuliwa kwa Palestina ni sawa na kukubali ugaidi, huku ikikabiliwa na shinikizo la kimataifa la kusitisha vita vinavyoendelea Gaza. Taarifa ya Wizara ya Afya inayoendeshwa na Hamas imesema tangu Jumamosi iliyopita watu watano wamefariki dunia kutokana na njaa na utapiamlo huko Gaza, na idadi ya vifo kufikia 217.
Aidha, tangu kuanza kwa mashambulizi ya kijeshi ya Israel mwaka 2023, zaidi ya watu 61,000 wamepoteza maisha. Mashambulizi hayo yalizuka kufuatia uvamizi mkubwa ulioongozwa na kundi la Hamas Oktoba 7, 2023, ambapo watu wapatao 1,200 waliuawa na wengine 251 kuchukuliwa mateka.
Kwa upande wake, Mamlaka ya Palestina inayosimamia baadhi ya maeneo ya Ukingo wa Magharibi imesema hatua hiyo ni ishara ya kuongezeka kwa uungwaji mkono wa kimataifa kwa haki ya Wapalestina ya kujitawala. Waziri Mkuu Albanese alieleza kuwa uamuzi wa serikali yake umetokana na ahadi ya Rais wa Mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas, kuwa Hamas haitakuwa na nafasi katika uongozi wa taifa la Palestina litakapoundwa.
Hatua hiyo pia ni matokeo ya mashauriano ya karibu kati ya Australia na viongozi wa mataifa mengine, yakiwemo Uingereza, Ufaransa, New Zealand na Japan, yaliyofanyika katika kipindi cha wiki mbili zilizopita. “Tunaamini huu ni wakati wa fursa ya kihistoria, na Australia iko tayari kushirikiana na jumuiya ya kimataifa kuitumia ipasavyo,” alisema Albanese.