AUWSA yapongezwa usimamizi mradi wa maji

MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Arusha (AUWSA) imepongezwa kwa kusimamia vyema mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya Sh bilioni 520 ambao umetatua changamoto za maji kwa wananchi.

Aidha Bodi ya AUWSA imeagizwa kuchukua hatua kwa wananchi wanaoharibu miundombinu ya maji.

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Amir Mkalipa amezungumza hayo leo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda wakati wa uzinduzi wa Bodi ya 10 ya Wakurugenzi wa AUWSA na kusisitiza serikali imeridhishwa na ufanisi wa kazi ya mamlaka hiyo.

Advertisement

Amesema uwepo wa bodi hiyo utasaidia serikali kufanya kazi na kusisitiza uzalendo, uaminifu na uadilifu kwani wananchi wanahitaji maji ili kuendelea na shughuli zao za kimaendeleo ikiwemo Auwsa kuongeza zaidi idadi ya wateja na kusambaza mtandao wa maji kata kwa kata.

“Endeleeni kuongeza idadi ya wateja ikiwemo ongezeko la makusanyo kila mwezi uakiongezeka kutoka Sh bilioni1. 8 hadi kufikia sh, bilioni 2.4 ”

Pia aliipongeza bodi iliyopita kwa kupata hati safi kutokana na usimamizi mzuri wa miradi, huduma za maji, kitengo cha huduma kwa wateja huku akisisitiza maendeleo hayakosi changamoto kwa baadhi ya wananchi kuharibu miundombinu ikiwemo kuziba kwa makusudi mtandao wa maji taka.

Awali, Mkurugenzi wa Auwsa , Mhandisi Justine Rujomba alimpongeza Waziri wa Maji, Jumaa Aweso kwa ushirikiano mkubwa anaotoa katika mamlaka hiyo

inaendelea kukua na kuleta kuwa utekelezaji wa usambazaji wa maji katika Jiji la Arusha umewezesha mtandao wa kusambaza maji na kufikia asilimia 99 ikiwemo miji midogo ya Mererani, Longido, Monduli na Usa river.