Aweso ataka weledi utekelezaji wa miradi

ARUSHA: Waziri wa  Maji, Jumaa  Aweso amewataka watendaji wa Wizara ya Maji kutekeleza miradi kwa weledi, viwango  na kuzingatia uadilifu.

Waziri Aweso amesema hayo wakati akifungua Mkutano wa wadau wa Sekta ya Maji katika  Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano (wa  AICC) Jijini Arusha, ambao unafanyika  kwa siku mbili na kutaka Sekta Binafsi ipewe kipaumbele kama mdau mkuu katika kufanikisha masuala ya maji katika jamii.

Advertisement

Mkutano wa Wadau wa Sekta ya Maji, umeitishwa na Wizara ya Maji ukiwa na lengo la kuwashukuru wadau mbalimbali wa sekta ya maji kwa mchango wao mkubwa katika kuwezesha mafanikio yaliyopatikana katika sekta hiyo nchini.

Pia,Sambamba na hilo, wadau watapata fursa ya kujadili na kutoa maoni na mapendekezo kuhusu Rasimu ya Sera ya Taifa ya Maji ya mwaka 2002, toleo la mwaka 2023 na mpango mkakati wa wizara.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Prof. Jamal Katundu akizungumzia mkutano huo amesema maoni na mapendekezo  ya wadau wa sekta ya maji ni muhimu sana katika kuandaa Sera ya Taifa ya Maji ya mwaka 2002, toleo la 2023 katika kutekeleza dhana ya ushirikishwaji.

 

 

 

 

1 comments

Comments are closed.