Azam yang’ara Afrika

DAR ES SALAAM; TIMU ya soka ya Azam FC imeng’ara kwa kusonga mbele katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya leo kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya El Merriekh Bentiu ya Sudan Kusini mchezo uliofanyika Uwanja wa Azam Chamazi, Dar es Salaam.
Azam FC sasa imesonga mbele kwa jumla ya mabao 4-0 baada ya mchezo wa kwanza kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 nchini Sudan.