Bakwata yapongeza kuimarisha umoja, amani

DAR ES SALAAM: Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limepongezwa kwa kuimarisha amani, umoja na mshikamano nchini.

Pongezi hizo zimetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusianao, Deus Sangu wakati wa ziara yake ya kikazi katika Makao Makuu ya Baraza hilo Januari 03, 2025 jijini Dar es Salaam.

Ziara hiyo imelenga kujitambulisha kwa viongozi wa baraza hilo pamoja na kulitambulisha rasmi jukumu jipya la uhusiano ambao Ofisi ya Waziri Mkuu imekabidhiwa kuratibu.

Akizungumza katika kikao hicho, Waziri Sangu ameipongeza BAKWATA kwa mchango wake mkubwa katika kudumisha amani, umoja na mshikamano wa kitaifa.

Aidha, ameeleza kuwa baraza hilo limekuwa nguzo muhimu ya maadili na mshikamano wa kijamii kwa kuhimiza mazungumzo ya amani, kuvumiliana na kuimarisha mahusiano mema baina ya waumini wa dini mbalimbali.

“Juhudi hizi zimechangia kwa kiasi kikubwa kudumisha utulivu na mshikamano wa kitaifa,” alisema Waziri Sangu.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na taasisi za kidini katika kushughulikia changamoto za kijamii, kiuchumi, kisiasa, kikanda na kimataifa, hususan katika eneo la malezi bora na ujenzi wa jamii yenye maadili mema.

Sambamba na hayo, Waziri Sangu ameihakikishia BAKWATA kuwa Serikali itaendelea kushirikiana kwa karibu na baraza hilo pamoja na taasisi nyingine katika kuendeleza agenda ya amani, mshikamano na maendeleo jumuishi.

Kwa upande wake, Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir bin Ally amempongeza Rais Samia kwa kutambua umuhimu wa masuala ya Mahusiano na kuanzisha Wizara mahsusi inayoratibu eneo hilo.

Aidha, ameishukuru Serikali kwa kutambua na kuthamini mchango wa BAKWATA na kuahidi kuwa naraza hilo litaendelea kushirikiana na Serikali katika kuimarisha umoja wa kitaifa, amani na mshikamano nchini.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. l Get paid over $110 per hour working from home. l never thought I’d be able to do it but my buddy makes over $21269 a month doing this and she convinced me to try. The possibility with this is endless….

    This is what I do………………………………….. https://Www.Cash54.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button