Balozi Luhemeja amkabidhi ofisi Dk Muyungi

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dk Richarid Muyungi amekabidhiwa ofisi na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Balozi Mhandisi Cyprian Luhemeja, Dodoma, leo Januari 14, 2025.

Dk Muyungi ameahidi kuyaendeleza yale mazuri yaliyokuwa yamefanywa na mtangulizi wake kuhakikisha wanafikia lengo la ofisi katika uhifadhi na utunzaji wa mazingira, masuala yanayohusu Muungano pamoja na masuala ya Uchumi wa Buluu.

Kwa upande wake, Balozi Luhemeja ameishukuru menejimenti na watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kumpa ushirikiano wakati akiwa Katibu Mkuu katika kurahisi kazi kwenye utendaji.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button