Balozi Marekani afanya ziara Mtwara

MTWARA: KAIMU Balozi wa Marekeni nchini Tanzania, Andrew Lentz ametembelea Mkoa wa Mtwara kwa shughuli mbalimbali za kidiplomasia.
Balozi huyo akiwa ameambatana na ujumbe maalum amefika Mtwara kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa, Kanali Patrick Sawala namna wananchi wa Mtwara kupitia Tanzania wanaweza kushirikiana na Marekeni kukuza uchumi, na maendeleo ya Mtwara.

Baada ya mazungumzo, Balozi Lentz na ujumbe wake walitembelea Bandari ya Mtwara kujionea maendeleo ambayo yamefanywa na Dk Rais Samia Suluhu kwenye bandari hiyo.

“Raisi Dk. Samia Suluhu Hassan ameendelea kufungua Mtwara, amewekeza fedha nyingi katika Bandari yetu, na inaendelea kuwavutia waheshimiwa mabalozi kutoka nchi mbalimbali ili kuona na kushawishi wawekezaji kutoka kwenye nchi zao kuja kuwekeza,” amesema.



