Balozi Omar aitaka GBT kudhibiti madhara katika jamii

WAZIRI wa Fedha Balozi Khamis Mussa Omar ameitaka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini (Gaming Board of Tanzania) kuhakikisha inasimamia vema sekta hiyo ili kudhibiti madhara katika jamii hususan kwa vijana.

Balozi Omar ametoa rai hiyo jijini Dodoma alipokutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe wa Bodi hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Balozi Mstaafu Modest Jonathan Mero, kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Bodi.

Amesema kuwa, michezo ya kubahatisha imeruhusiwa kisheria imekuwa na mchango mkubwa katika kukuza pato la Taifa lakini ni muhimu ikaendelea kusimamiwa vizuri.

“Bodi ya Michezo ya Kubahatisha inatakiwa kutafuta utaratibu maalumu ambao utasaidia kudhibiti michezo inayokiuka Sheria zilizowekwa kwa kushirikiana na wadau wengine, kwa kuwa michezo hiyo iliyopo hadi vijijini vijana wanatumia muda mwingi kwenye michezo bila kufanya kazi”, amesema Balozi Omar.

Aidha ameitaka Bodi hiyo kuendelea kutoa elimu kwa wadau mbalimbali ili kuwa na uelewa wa michezo hiyo ili wacheze kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa bila kuathiri maadili ya umma.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Nchini, Balozi Mstaafu Modest Jonathan Mero alisema kuwa, michezo hiyo imekuwa na mchango mkubwa katika pato la Taifa ambapo mapato yamekuwa yakipanda kutoka shilingi bilioni 130 mwaka 2021/2022 hadi kufikia shilingi bilioni 260 mwaka 2024/2025.

Aidha, amesema kuwa Sekta hiyo imeajiri takribani watu 30,000 ambao ni wadau wanaoendesha michezo hiyo na pia imekuwa ikitoa michango kwenye sekta ya michezo ikiwemo kudhamini mchezo wa mpira wa miguu.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha hapa nchini, James Mbalwe, alisema kuwa Sekta hiyo imechangia kwa kiasi kikubwa katika Mfuko Mkuu wa Serikali ambapo kwa miaka mitano imechangia zaidi ya shilingi bilioni 900 na michango inaendelea kuongezeka kila mwaka.

Mbalwe aliwaonya watu wanaoendesha michezo hiyo ya kubahatisha kwa njia haramu ikiwemo kumiliki mashine za kuchezeshea kamali-Madubwi (Slot Machines) ambazo hazijasaliwa kuacha tabia hiyo mara moja na kwamba hatua kali zitachukuliwa kwa watu wanaojihusisha na vitendo hivyo kwa kushirikiana na Mamlaka za Serikali za Mitaa-TAMISEMI.

“Nataka kuwaambia pia watanzania hususani vijana kuwa sekta hii ni burudani na sio mbadala wa kufanya kazi, ni lazima wafanye kazi wapate fedha wakaburudike”, alisema Mbalwe.

Bodi ya Michezo ya Kubahatisha ilianzishwa mwaka 2003 kwa madhumuni ya kusimamaia urekebu wa michezo hiyo nchini.

Habari Zifananazo

7 Comments

    1. I just came across this amazing way to earn $6,000-$8,000 a week online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
      .
      Follow Here ……………………… https://Www.Cash54.Com

    2. I am making a real GOOD MONEY (300$ to 400$ / hr )online from my laptop. Last month I GOT check of nearly 18,000$, this online work is simple and straightforward, don’t have to go OFFICE, Its home online job. At that point this work opportunity is for you.if you interested.simply give it a shot on the accompanying site….Simply go to the BELOW SITE and start your work…

      .
      M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com

  1. I make up to $90 an hour working from my home. My story is that I quit working at Walmart to work online and with a little effort I easily bring in around $40h to $86h… Someone was good to me by sharing this link with me, so now i am hoping i could help someone else out there by sharing this link…
    Try it, you won’t regret it!….. http://www.hot.cash54.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button