Bandari kavu, kongani ya viwanda Kwala vichochee ukuaji uchumi

LEO Rais Samia Suluhu Hassan anaweka jiwe la msingi la ujenzi wa Kongani ya Viwanda Kwala pamoja na kufungua bandari kavu ya Kwala wilayani Kibaha, Pwani, pamoja na uzinduzi wa treni ya mizigo ya SGR.

Katika Kongani ya Viwanda Kwala, tayari viwanda saba vinafanya kazi na vitano vikiwa katika hatua za mwisho za ujenzi. Kongani hiyo yenye thamani ya Dola za Marekani bilioni tatu, imejengwa katika eneo lenye ukubwa wa ekari 2,500.

Aidha, inalenga kuwa na zaidi ya viwanda 200 hatua inayotarajiwa kuimarisha kwa kiasi kikubwa maendeleo ya sekta ya viwanda nchini. Pia hatua hiyo itaongeza ufanisi wa usafirishaji wa bidhaa kwenda masoko ya ndani na nje ya nchi.

Kwa mujibu wa Jafo, mradi huo mkubwa unatarajiwa kutoa ajira zaidi ya 50,000 za moja kwa moja na ajira zisizo za moja kwa moja zipatazo 150,000 kwa Watanzania. Tayari watu 311 wamekwishapata ajira kupitia shughuli zinazoendelea hapo.

Kwa upande wa bandari kavu ya Kwala, inatarajiwa itakuwa na bandari kavu tisa za nchi jirani zinatumia Tanzania kama lango kuu la kusafirisha bidhaa.

Uzinduzi wa Bandari ya Kwala na ubebaji mizigo kupitia treni ya SGR na bandari hiyo utapunguza mrundikano wa mizigo Bandari ya Dar es Salaam kwa asilimia 30.

Tungependa kuipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Samia kwa kuendelea kuifungua nchi kwa miradi mikubwa ya kimkakati kama hii ya kongani ya viwanda na bandari kavu ya Kwala na treni ya mizigo ya SGR.

Miradi yote hii ni kielelezo na uthibitisho wa dhahiri wa maono ya Rais Samia ya kuhakikisha Tanzania inapiga hatua kubwa za kimaendeleo kwa kutumia fursa ilizo nazo na zile zinazozunguka nchini kama vile kuzungukwa na nchi jirani ambazo zinaitumia Bandari ya Dar es Salaam kama lango lao la biashara.

Serikali pia inastahili pongezi kwa sababu miradi hii inaifungua bandari kwa masoko ya kimataifa na kuongeza ushindani dhidi ya bandari za nchi jirani.

Tunaamini kama ilivyoelezwa hapo juu kuwa miradi hii mbali ya kupunguza foleni na mlundikano wa bidhaa katika Bandari ya Dar es Salaam, lakini inakwenda kuwa kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi kwa kuongeza mapato ya taifa, kuongeza ajira nchini, kulinda barabara na kuimarisha sekta za viwanda na usafirishaji.

Wakati anapotarajiwa kuzindua miradi hii leo, hatuna shaka kwamba Watanzania watazidi kumuunga mkono Rais Samia na serikali yake katika azma ya kuboresha maisha yao kupitia miradi ya maendeleo, na kubwa wanalopaswa kulifanya ni kuhakikisha nchi inabaki katika amani na utulivu ili maendeleo yafanyike.

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. I get paid over $130 1 to 3 hours working from home with 2 kids at home. I never thought I’d be able to do it but my best friend earns over $27k a month doing this and she convinced me to try. The potential with this is endless.

    Heress———–> http://www.best.work43.com

  2. My spouse and I stumbled over here by a different website and thought I might as well check things out. I like what I see so i am just following you. Look forward to checking out your web page again.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button