Bandari yachangia 40% Pato la Taifa

WIZARA ya Uchukuzi imesema sekta ya usafirishaji kupitia bandari inachangia asilimia 40 ya mapato ya nchi.
Pia, imesema serikali ina matarajio ya kuunganisha bandari na Reli ya Kisasa (SGR) ili kuwa na uchumi fungamanishi na kurahisisha shughuli za usafirishaji.
Mkurungezi wa Miundombinu kutoka Wizara ya Uchukuzi, Shomari Shomari ameeleza hayo wakati wa Kongamano la Kitaifa la Wadau wa Uchumi wa Buluu 2025 lililofanyiaka mkoani Dar es Salam.
Kongamano hilo la nne kufanyika limeandaliwa na Chuo cha Bahari cha Dar es Salaam (DMI), kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira na Wizara ya Uchukuzi ili kuangazia fursa zilizopo katika uchumi wa buluu na namna ya kuzitumia kwa maendeleo endelevu.
SOMA: Rais Samia atoa msimamo bandari
Akizungumza katika kongamano hilo, Shomari amesema bandari ina fursa kubwa kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja na kwa taifa kwa ujumla.
“Kwenye usafirishaji zipo fursa za kiuchumi. Hata kwa upande wa serikali, kwenye upande wa ukusanyaji wa mapato kwenye sekta ya usafirishaji, bandari ndio kunakotegemewa kwa kiasi kikubwa. “Namba zinasema karibu asilimia 40 ya mapato ya nchi yanatokana na bandari, ukiacha yale mwengine,” amesema.
Amesema uchumi wa buluu umegawanyika katika sekta nyingi kuanzia kwenye uvuvi, usafirishaji, utalii na utafiti.
Tanzania imebarikiwa kuwa na bahari, maziwa makuu na mito inayochangia kukuza mnyororo wa usafirishaji kutoka Tanzania na nchi nyingine zinazoizunguka.
Naye Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Abdallah Hassan Mitawi akifungua kongamano hilo amesema rasilimali za bahari zikitumika ipasavyo zitaongeza nafasi za ajira, kukuza biashara na usafirishaji, utalii na nishati jadidifu.
Mitawi amesema serikali imeendelea kuweka msisitizo katika uchumi wa buluu ikiwemo kuboresha bandari ili kuimarisha usafirishaji, kuimarisha sekta ya uvuvi, kuweka miongozo ya usalama baharini na kuimarisha ushirikiano kikanda na kimataifa.
Amesema Umoja wa Ulaya umetoa Euro milioni 370 kwa benki kuwakopesha wadau wa uchumi wa buluu ili kusaidia miradi ya uchumi wa buluu katika taasisi mbalimbali.
Mitawi amesema ili kufanya uchumi wa buluu kuwa na tija katika kuchangia uchumi wa nchi vijana, wanawake na sekta binafsi ni wadau muhimu wanaopaswa kupewa kipaumbele katika sera na mafunzo ili washiriki kikamilifu.
“Kupitia sera ya uchumi wa buluu iliyozinduliwa na malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo, serikali inakusudia uchumi wa buluu kuwa sekta kiongozi katika kuchangia uchumi na pato la taifa,” amesema.
JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12000 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com
Easy now to earn extra cash per month simply doing work from home. change your life completely and makes it better than ever. earns more than $27k every month simply doing online job for 3 or 4 hours a day. i made $22694 from this by working online in last month. details on this website…..
COPY THIS→→→→ http://Www.Cashprofit7.site
I just got paid $22k working off my laptop this month!** And if you think that’s cool, my divorced friend has twin toddlers and made over $22620 her first month.details on this website**Want the secret?** Copy this Website and choose HOME TECH OR MEDIA……..
Here is I started_______ https://Www.Jobathome1.Com
I just got paid $22k working off my laptop this month!** And if you think that’s cool, my divorced friend has twin toddlers and made over $22620 her first month.details on this website**Want the secret?** Copy this Website and choose HOME TECH OR MEDIA……..
Here is I started_______ https://Www.Jobathome1.Com