Bandari Zanzibar mabingwa wapya wa soka ‘interpplort games 2025’

TIMU ya soka ya Shirika la Bandari Zanzibar (ZPC),imetwaa ubingwa wa Michezo ya 18 ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) “InterPort Games 2025” kwa mara ya kwanza kwa kuifunga Dar es Salaam Port kwa bao 1-0 katika mchezo wa fainali uliofanyika uwanja wa Jamhuri Morogoro
Katika miaka 18 ya mashindano hayo, Shirika la Bandari Zanzibar limeshiriki mara 16 na timu hiyp ilifanikiwa kucheza fainali mara mbili kwa miaka tofauti na kuambulia nafasi ya pili.
Bao hilo lililowapa ubingwa wa mara ya kwanza tangu kushiriki mashindano hayo lilipachikwa kwa mkwaju wa penati na mchezaji Mohammed Kombo Juma kwenye kipindi cha pili cha mchezo ambao ululichezeshwa kwa dakika 60.
Mlinzi wa timu hiyo ,Mohammed Makame Kibanda alishukuru kwa kumaliza mchezo wa fainali kwa usalama na kueleza kuwa siri ya ushindi huo ulitokana na wachezaji kufuata maelekezo ya mwalimu wao.

“Mchezo ulikuwa wenye ushindani mkubwa , kutokana na kuyafanyia kazi maelekezo ya mwalimu wetu tumepata ushindi wa kutwaa taji , hii ni mara ya kwanza kutwaa kombe ingawa misimu mwili mfufulizo tumecheza fainali ila hatukufanikiwa kuchukua kombe , isipo kuwa msimu huu Mungu ametujalia tumechukua kombe” alisema Kibanda.
Timu zingine zilizotwaa ubingwa katika mchezo wa Netiboli ni Shirika la Bandari Zanzibar, Bandari ya Tanga ikinyakua mchezo wa mpira wa kikapu ,Bandari ya Dar es Salaam ikitwaa ubingwa wa mpira wa wavu kwa upande wa wanaume na wanawake pamoja na kutwaa ushidni wa jumla.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Wakili Plasduce Mbossa, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano, Mbarikiwa Masinga, aliipongeza kamati ya maandalizi, waamuzi na washiriki wote kwa nidhamu na moyo wa kushindana waliouonyesha katika kipindi chote cha mashindano.
Katika ujumbe wake, Wakili Mbossa alisisitiza kuwa michezo hiyo ni zaidi ya ushindani, kwani huimarisha afya, mshikamano na utayari wa watumishi katika kutekeleza majukumu yao kwa weledi na ufanisi mahala pa kazi.
Licha ya hayo aliwataka watumishi wote wa TPA na sekta ya bandari kwa ujumla kushiriki kikamilifu katika zoezi la kupiga kura Oktoba 29, 2025, akieleza kuwa ni wajibu wa kila mtumishi na raia kushiriki katika mchakato huo wa kidemokrasia kwa amani na utulivu.
Michezo hiyo ilianza Oktoba 22 hadi 24, mwaka huu na ilishirikisha wanamichezo 636 kati yao, 466 ni kutoka TPA, 95 kutoka ZPC ,52 kutoka DP WORLD Dar es Salaam na 23 kutoka Kampuni ya Meli Tanzania (TASHICO), ikiwa na kauli mbiu: “Michezo ya Bandari 2025 kwa afya, tija na mshikamano kwa wafanyakazi; tujitokeze kupiga kura Oktoba 29” .




JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com
I get paid over 220 Dollars per hour working from home with 2 kids at home. i never thought i’d be able to do it but my best friend earns over 15k a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life. This is what I do, check it out by Visiting Following Website
Open This…. http://Www.Work99.Site
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com
My pay at least $300/day.My co-worker says me!I’m really amazed because you really help people to have ideas how to earn money. Thank you for your ideas and I hope that you’ll achieve more and receive more blessings. I admire your Website I hope you will notice me & I hope I can also win your paypal giveaway…….. https://cashprofit7.site