DAR ES SALAAM: MAHAKAMA ya Wilaya ya Kinondoni imemhukumu Baraka Benedictor ,22, mkazi wa Sinza, kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti kijana wa kiume mwenye umri wa miaka 14.
Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Nambwike Mbaba, ambaye alieleza kuwa mahakama imejiridhisha na ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri. Ushahidi huo ulithibitisha bila shaka yoyote kwamba mtuhumiwa alitenda kosa hilo.
Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, Baraka alitenda kosa hilo mnamo Februari 3, 2024, katika eneo la Sinza Lion, wilayani Kinondoni, ambapo alimlawiti kijana huyo kinyume na maumbile. Tukio hilo liliripotiwa na kufanyiwa uchunguzi uliosababisha kufunguliwa kwa kesi dhidi ya mtuhumiwa.
Baraka Benedictor alishtakiwa kwa mujibu wa Kesi Namba 5866/2024, chini ya kifungu cha 154(1)(a) na (2) cha Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 Marejeo ya Mwaka 2022. Kifungu hiki kinabainisha adhabu kali kwa makosa ya ulawiti, hasa yanapohusisha watoto.
Baada ya kusikiliza pande zote, Mahakama iliona kuwa ushahidi wa upande wa mashtaka ulikuwa wa kutosha na hivyo ikatoa adhabu ya kifungo cha miaka 30 jela kwa mtuhumiwa, hatua inayotajwa kuwa fundisho kwa wengine wenye nia ya kutenda makosa ya aina hiyo.
Sakarya Elit Escort Kızlarla Vip Bayanlar Esort Güzel Vakit Geçirin