Basata yatangaza punguzo la tozo kwa wasanii

DAR ES SALAAM: BARAZA la Sanaa Tanzania (BASATA) limetangaza punguzo la tozo za usajili wa wasanii na vibali kutoka Sh 40,000 hadi Sh 20,000 ambapo usajili binafsi wa msanii utakuwa Sh 10,000 badala ya Sh 20,000 ya awali.

Akizungumza na waandishi wa habari Jana Jijini Dar es Salaam Katibu Mtendaji wa barazahilo Dk Kedmon Mapana amewataja wengine waliopunguziwa gharama hizo ni waendesha shughuli za muziki (ma-dj’s) ambao wamepunguziwa kutoka kulipa Sh 40,000 hadi Sh10,000.

Vingine vilivyopunguzwa ni tozo kwa wasanii wanaotoka nje ya nchi kwa sasa watatakiwa kulipa Sh 250,000 badala ya Sh milioni 1 ya awali na wanaoendesha shughuli mbalimbali zikiwemo matamasha watatakiwa kulipa Sh 50,000 kulingana na bei za viingilio wanavyoweka.

Dk Mapana amesema maboresho hayo yanatokana na maboresho ya kanuni ya mwaka 2019 yanayolenga kupata wasanii wengi zaidi watakaojisajili.

Aidha amewataka wasanii wengi wajisajili Baraza la Sanaa kwa kuwa sasa tozo zimepunguzwa kwa asilimia kubwa.

Akizungumzia vipengele vilivyoongezwa katika usimamizi wa Baraza hilo ni pamoja na fani ya wanamitindo wakiwemo watu wa salooni za kike na kiume pamoja na waongoza muziki (ma-dj’s).

Habari Zifananazo

Back to top button