Vijana washauriwa kusoma masomo ya sanaa

DAR ES SALAAM: VIJANA wametakiwa kusoma masomo ya sanaa kwa kuwa ni  nyenzo muhimu katika kuitangaza nchi, pamoja na kutoa ajira na kuongeza mahusiano na utamaduni wa nchi nyingine.

Hayo yamesemwa na Ofisa Uhusiano kwa Umma kutoka Kituo cha Utamaduni cha Iran, Amani Salum amesema kwa pamoja kati ya chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kituo hicho wamejifunza pamoja kuhusu tamaduni mbalimbali ikiwemo historia za nchi hizo mbili.

Amesema pia wanakaribishwa wanafunzi wa vyuo vingine ili waweze kujifunza.

“Tupo hapa kwaajili ya kuchanganya tamaduni na kujifunza za wengine kwa kubadilishana mawazo,” amesema.

Zaidi ya kujifunza tamaduni mbalimbali, lakini wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam waliweza kushindanisha michoro mbalimbali ambayo waliibuni .

Juhudi ya Pamoja kati ya Kituo cha Utamaduni cha Iran na Idara ya Sanaa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, yenye kauli mbiu “Kwa Macho Mengi kwa Ubinadamu,” imebainisha imani kwamba ubinadamu ni njia ya maisha.

Sanaa na utamaduni vina jukumu la kuonyesha umuhimu wa ubinadamu kama thamani ya pamoja.

Hivyo, tunaweza kuunda mazingira, jinsi tunavyoweza kutunza wanyama, na jinsi sisi wanadamu tunavyotendeana. Bila kujali rangi zetu, utaifa wetu, lugha zetu, au dini zetu. Hii ndiyo sababu tumechagua kauli mbiu hii, njia nyingi kwa ubinadamu, na kupitia mpango mzima, tumepokea mazuri mengi.

Mshiriki katika tamasha hilo Tukuswiga Samson, amesema sanaa ni pana, hivyo amewataka vijana wenzake waweze kujiwekeza katika sanaa ili waweze kujipatia kipato

“Sanaa ni pana sana inaweza kumsaidia na kumpa kipato kijana yoyote ambaye ataamua kuichukilia kwa umakini”  amesema Tukuswida Samson.

Mwalimu Msimamizi ,Erick Mgema  ameiomba serikali kuongeza nguvu kwa wadau wa taasisi za tamaduni, kwakuwa wao ndio wanaweza kufikisha kwa wananchi wengi na kuongeza idadi ya wanafunzi wa masomo ya sanaa.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button