Bashungwa: Hakuna atakayethubutu kuandamana Okt 29

KAGERA: MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Karagwe na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amewaondoa shaka Watanzania akisisitiza uhakika wa uwepo wa usalama wa kutosha katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu.

Akizungumza wakati wa mkutano wa mgombea urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi ( CCM) wilayani Karagwe mkoani Kagera leo Oktoba 15, Bashungwa amesema vyombo vya usalama vinaendelea na majukumu yake kuhakisha amani ya nchi inaendelea kuwepo.

“Ninaomba niwahakikishie wana Karagwe na Watanzania kwa ujumla kuwa tangu Rais unipe jukumu la kuisimamia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, vyombo vyote vya ulinzi na usalama vinaendelea kufanya kazi kwa weledi mkubwa ili kuhakiksha amani ya Tanzania inaendelea kutamalaki” amesema Bashungwa na kuongeza

Hakutakuwa na mtu yoyote atakayethubutu kuandamana Oktoba 29 atakayefanya hivyo atakutana na kisiki, niwaombe vijana wa Tanzania msikubali kuingia kwenye mkumbo huo tuendelee kushirikiana katika kulijenga taifa letu” amehitimisha Bashungwa

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button