Benki, DSE wafanikisha ugawaji tuzo 2024

BENKI ya Mwanga Hakika kwa kushirikiana na Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) imefanikisha utoaji wa tuzo za wanachama wa DSE kwa mwaka 2024, zikihusisha makampuni, mabenki, na viwanda vilivyokidhi vigezo vya utendaji bora.

Kampuni ya Orbit Securities ilijinyakulia tuzo mbili, ikiwemo tuzo ya “Best Broker of the Year 2024,” kutokana na juhudi zake katika mazingira, jamii, na utawala (ESG).

Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Orbit Securities, Godfrey Gabriel alisema kuwa tuzo hizo zitachochea kampuni kuongeza juhudi za kutoa elimu kwa jamii kuhusu masuala ya uwekezaji, ili kuwahamasisha Watanzania kuwekeza kwenye masoko ya mitaji kwa ajili ya kukuza uchumi.

Advertisement

Naye Innocent Yonazi Mkuu wa Idara ya Uhusiano kwa wawekezaji NMB amefurahishwa na tuzo hizi ambapo walipata tuzo nne.

Tuzo hizo ni pamoja na kampuni bora ya mabenki, mtunza mali wa mwaka,mtoa hati fungani, muuzaji wa hati fungani bora,

Kwa niaba ya Mkurugenzi wa Benki ya Mwanga Hakika, Mwinyimkuu Ngalima alisisitiza dhamira ya benki hiyo kuendelea kuwaunga mkono wanachama wa DSE katika kujenga soko jumuishi lenye matarajio bora kwa siku zijazo.