Bessent, He Lifeng wakutana Stockholm

STOCKHOLM, USWIDI : SERIKALI ya Marekani na China zimeingia katika siku ya pili ya mazungumzo ya ngazi ya juu jijini Stockholm, Sweden, yanayolenga kupunguza mvutano wa muda mrefu wa kibiashara kati ya mataifa hayo mawili makubwa kiuchumi duniani.

Waziri wa Fedha wa Marekani, Scott Bessent, na Naibu Waziri Mkuu wa China, He Lifeng, wanaongoza mazungumzo hayo. Hata hivyo, hadi sasa hakuna taarifa rasmi iliyotolewa kuhusu maudhui au makubaliano ya awali yaliyofikiwa katika siku ya kwanza ya mazungumzo hayo. SOMA: Vitisho vya Marekani havinitishi

Wachambuzi wa masuala ya uchumi wanasema kuna uwezekano wa kuongezwa kwa viwango vya ushuru wa bidhaa iwapo mazungumzo hayo hayataweza kukamilika. Serikali ya Marekani imekuwa ikirekebisha makubaliano ya ushuru na mataifa mbalimbali tangu Rais Donald Trump alipoongeza ushuru wa bidhaa kwa baadhi ya nchi mwezi Aprili.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button