Bil 20/- zatekeleza miradi ya maendeleo Bakoba

BUKOBA: KIASI cha Sh bilioni 20.6 zimetumika kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwemo ukarabati wa bandari iliyopo katika kata ya bakoba Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), diwani wa kata hiyo, Shabani Rashid amesema serikali imetekeleza miradi mikubwa inayogusa jamii.

Amesema kuna mabadiliko makubwa katika miradi ya barabara, afya, maji, elimu ambayo moja kwa moja imengusa mwananchi mmoja mmoja na kuchochea maendeleo katika kata hiyo.
SOMA ZAIDI: Diwani Mutayoba atoa somo uchaguzi serikali za mtaa,vijiji
Amesema kuwa anapoelekea kumaliza miaka mitano ameshuhudia mabadiliko makubwa katika uunganishwaji na ufunguzi wa barabara nyingi katika kata hiyo ambazo hazijawahi kufunguliwa na sasa wananchi wanamasiliano mazuri ya barabara, ukarabati wa shule ya zamani ambayo ilijengwa kwa tope ,ukarabati wa maabara ya kemia ,ujenzi wa madarasa, vyoo bora ,uwepo wa maji safi na salama ya bomba ukilinganisha na miaka iliyopita.

“Kata hii ilikuwa chini ya upinzani kwa miaka 15,kama kijana nilipewa dhamana ya kuongoza kata hii , serikali imefanya mambo makubwa sana ambayo hayajawahi kushuhudiwa hivyo wananchi wanafurahia na Imani kati ya wananchi na serikali yao imeongezeka,” amesema Rashid.

Alisema maono yake makubwa ni kuhakikisha miradi ya maendeleo inaendelea kutekelezwa,wananchi kupata huduma nzuri kiafya,miradi ya ujenzi ya kingo za mto kanoni zinatekelezeka pamoja na kuona jamii ya vijana inayoendelea kukua kwa maadili na kuwa na maono ambayo yanalenga kuleta maendeleo kwa kila mtu.



