Bilioni 192 zatengwa miradi ya maendeleo Temeke

DAR ES SALAAM: BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Temeke limepitisha rasimu ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2026/2027 yenye jumla ya Shilingi bilioni 192, ambazo zinatarajiwa kutumika katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo elimu, barabara, afya pamoja na mikopo kwa makundi maalumu.
Rasimu hiyo ilipitishwa leo, Februari 19, 2026, jijini Dar es Salaam, wakati wa mkutano wa baraza la madiwani uliiongozwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Temeke, Uzairu Abdul, ambaye amesema bajeti hiyo inajumuisha fedha kutoka makusanyo ya ndani ya manispaa na fedha nyingine kutoka ruzuku ya serikali kuu.
Meya Abdul amesisitiza kwamba rasimu hiyo imepitishwa ili kukidhi matarajio makubwa ya wananchi wa manispaa hiyo, na kuongeza kuwa baraza lina jukumu la kusimamia fedha hizo kwa ufanisi ili kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa, huku wananchi na walipakodi wakihamasishwa kwamba fedha wanazolipa zinaenda kwenye maendeleo.
“Tumeanza kujenga shule zaidi ya 5 za ghorofa. Katika elimu ya msingi, tuna shule nne za ghorofa zinazoendelea kujengwa maeneo mbalimbali ya Temeke. Kwa upande wa sekondari, tunajenga ghorofa nne, kila jengo litakuwa na ghorofa tano na vyumba kuanzia 54 na kuendelea,” amesema Meya Abdul.

Aidha, amesema kuwa katika sekta ya elimu, bajeti hiyo itatumika kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo mrundikano wa wanafunzi darasani, upungufu wa madawati na maabara. Katika sekta ya afya, ghorofa mbili zitajengwa ili kuboresha huduma za afya, na kwa upande wa barabara tumetenga fedha za kutosha kwa ajili ya matengenezo na ujenzi.
Kwa upande wake, Diwani wa Mbagala, Abdulkarim Pazi, amesema rasimu hiyo inalenga kuhakikisha manufaa kwa kata za Manispaa ya Temeke, na kwamba wananchi wanatarajia kuona mabadiliko makubwa ikiwemo miundombinu muhimu.




Barua hii nzuri deadcation yake
https://youtu.be/KzqoSeVMGrQ?si=5unaAkpHqOseFw2D
Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…
THIS→→→→ https://Www.FindJobs1.Site
I started this as a simple side hustle, and last month I made a little over $6,137 just working a few hours a day from my phone. If you want to check out how it works, the website has all the details.
Here—>> http://www.giftpay7.vip