KAGIS yagusa maisha ya Watanzania 123,000 mikoa 2
MRADI wa Uwezeshaji Wasichana Balehe kuendelea na Masomo (KAGIS) umesaidia takribani watu 123,489 katika mikoa ya Geita na Kigoma kwa miaka mitano ya utekelezaji.
Mradi wa KAGIS umetekelezwa chini ya usimamizi wa Shirika la Plan International pamoja na washirika wake ambao ni RAFIKI SDA na Shirika la WPC kwa ufadhili wa serikali ya Canada.
Mkurugenzi Mkazi wa Plan International Tanzania, Jane Sembuche ametoa taarifa hiyo wakati wa kufunga mradi wa KAGIS mkoani Geita.

Sembuche amesema miongoni mwa wanufaika hao ni wasichana, wavulana, wazazi, walezi, walimu na jamii ambao wameshiriki kwa dhamira thabiti na kufanya bidi ya kufikia mbadiliko.
Amesema ili kusaidia wasichana balehe kuhitimu masomo na kufikia malengo KAGIS imewajengea wasichana stadi za maisha na kuwezesha uchumi wa kaya kupitia vikundi akiba na mikopo.
Sembuche amesema kupitia ustahimilivu wa kaya, mradi wa KAGIS umefanikiwa kuwanufaisha wanawake 6,000 kupitia vikundi vya akiba na mikopo pamoja na kuwezesha wasichana 7,000 kubaki shule.

“Mradi umeonyesha matokeo makubwa katika mwitikio wa kijinsia kwa shule za msingi na sekondari kutoka kiwango cha awali cha asilimia 25 hadi asilimia 66 mwishoni mwa mradi.
“Haya ni matokeo ya mifumo bora ya ulinzi wa watoto, kuzuia ukatili wa kijinsia shuleni, kuwepo kwa maeneo salama kwa wasichana na kuimarika kwa uwajibikaji katika ngazi ya shule,” amesema.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela amesema KAGIS imeunga mkono juhudi za serikali katika kuimarisha sekta ya elimu kwa kujenga mazingira rafiki ya wasichana balehe kusalia shule.
Shigela amepongeza ufadhili wa serikali ya Canada katika mradi wa KAGIS huku akieleza kuwa hayo ni matokeo ya ushirikiano thabiti wa kidiplomasia baina ya Tanzania na serikali ya Canada.

Balozi wa Canada nchini Tanzania, Emily Burns amesema Canada inatambua umuhimu wa elimu hasa kwa watoto wa kike ndio maana iliguswa kuwawezesha mazingira rafiki ya kusoma shuleni.
Emily amesema mafanikio ya KAGIS ni hatua kubwa ya kuendeleza ushirikiano baina ya serikali ya Canada na Tanzania katika kufanikisha maendeleo ya sekta ya elimu katika jamii.




Barua hii nzuri deadcation yake
https://youtu.be/0t8OYCMXr_I?si=yCLzJ1zUmaWSa0py
I get paid over (90$ to 200$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $18000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
.
HERE——————————————⊃⫸ https://Www.Cash54.Com
I get paid over 220 Dollars per hour working from home with 2 kids at home. i never thought i’d be able to do it but my best friend earns over 15k a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life. This is what I do, check it out by Visiting Following Website…
.
More Details For Us→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com
Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…
THIS→→→→ https://Www.FindJobs1.Site