KIASI cha Sh bilioni 26 kinatarajia kutumika kwa ajili ya ujenzi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Kampasi ya Kigoma.
Mratibu wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Uchumi (HEET),Profesa Erasto Mbugi amesema kuwa ujenzi wa kampasi ya Kigoma unapaswa kukamilika Juni 2026.
Profesa Mbugi amesema kuwa ujenzi huo utahusisha jengo la utawala litakalotumiwa na watu 60, ukumbi wa mihadhara utakaochukua watu 150, maabara ya kompyuta, maktaba, maabara sita za kufundishia, bweni lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 111 na ukumbi wa mikutano wenye uwezo wa kuchukua watu 300,000 na uwanja wa michezo.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) wa pili kulia akisaini mkataba wa ujenzi wa chuo hicho na uongozi wa Kampuni ya China JIANGXI INTERNATIONAL AND TECHNICAL CO.LTD kwa ajili ya ujenzi wa chuo cha MUHAS Kampas ya Kigoma
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa chuo Kikuu Muhas, Profesa Appolinary Kamuhabwa akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Kigoma amesema kuwa wanafunzi 5900 wanatarajia kudahiliwa na chuo hicho kitakapokamilika.
Profess Kamuhabwa amesema kuwa ujenzi wa kampasi hiyo ya Kigoma unatoa fursa kubwa katika kutoa mafunzo na kufanya tafiti hasa eneo lililopo imepakana na nchi za ukanda wa maziwa makuu hivyo kufanya kuwa na fursa na nafasi kubwa ya kufanya tafiti za magonjwa.
Mkuu wa Mkoa Kigoma Thobias Andengenye akizungumza katika hafla ya utiaji saini kwa ajili ya ujenzi wa chuo cha MUHAS Kampasi ya Kigoma
Mkuu wa Mkoa Kigoma, Thobias Andengenye akihitimisha hafla ya utiaji saini wa ujenzi wa chuo hicho amesma kuwa ujenzi huo unatoa uhakikisho wa mkoa kuwa na uhakika wa kukabiliana na wataalam katika sekta ya afya ambapo ujenzi wa chuo na ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda vitachangia kufanya miradi hiyo kuwa sehemu ya utalii wa tiba kwa wageni wa ndani na nje ya nchi.