Bodaboda auawa kikatili Butiama
MWANAUME anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 36, ambaye hakufahamika kwa haraka amekutwa amekufa katika eneo la Maji machafu, Kijiji cha Nyabange Kata ya Nyankanga wilayani Butiama.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Longinus Tibishubwamu amesema wanaendelea na upelelezi wa tukio hilo, lakini taarifa za awali zinaeleza mtu huyo alikuwa akifanya shughuli za bodaboda mjini Musoma.
Ametaja chanzo cha kifo hicho kuwa ni tamaa ya mali, kwakuwa Pikipiki aliyokuwa akiiendesha iliibwa katika tukio hilo la Novemba 16 Mwaka huu.
Polisi imesema, marehemu alipigwa na kuchomwa na kitu chenye ncha kali kichwani, shingoni na tumboni na kumsababishia majeraha ambayo ndiyo yanayosadikiwa kumsababishia kifo.