TIMU nane za waendesha pikipiki (bodaboda) zimeanza kupambana katika ligi maalum kwa ajili ya kuhamasisha masuala ya usalama barabarani na masuala ya afya ya uzazi huku mshindi wa mashindano hayo akitarajia kuibuka na kitita cha Sh milioni
Mkurugenzi wa kituo cha Main FM Redio ambao ndiyo waandaji wa mashindano hayo, Pascal Willian amesema kuwa mashindano hayo yameandaliwa kwa ushirikiano wa redio hiyo, jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani Mkoa Kigoma na Hospitali ya Rufaa ya Kigoma Maweni.
Mkurugenzi wa Main FM Pascal William akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
Alisema kuwa mashindano hayo pia yatatumika kuhamasisha masuala ya uwekezaji ikiwa ni njia ya kufungua fursa za kiuchumi kwa watu mbalimbali watakaodhuria mashindano hayo na timu zinazoshiriki.
Mshindi wa pili anatarajia kuondoka na Sh 500,000 na kutakuwa na zawadi za washindi mbalumbali ikiwemo mchezaji bora.
Mashindano hayo yamefunguliwa na Mkuu wa Wilaya Kigoma, Dk.Rashid Chuachua ambaye aliwakilishwa na Ofisa Tawala wa Wilaya Kigoma, Dola Buzaire.
Mwakilishi wa kampuni ya gesi ya kupikia ya Oryx, Gibson Rodgers (kulia) akikabidhi mtungi wa gesi kwa mchezaji wa Kombaini ya Bodaboda Mlole ambaye alikuwa mchezaji bora wa mechi ya ufunguzi