BSS Msimu 16 Kuanza Februari 7

MASHINDANO makubwa ya kusaka vipaji nchini, Bongo Star Search (BSS) Msimu wa 16, yanatarajiwa kuanza rasmi Februari 7 na 8, 2026 jijini Mwanza, baada ya kuahirishwa kwa muda.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar-es-salaam, Januari 9, 2026, Mkurugenzi wa Bench Mark, Madam Rita Paulsen, amesema mashindano hayo yalicheleweshwa ili kuwapa waandaaji nafasi ya kujipanga vizuri na kuja na ubunifu mpana zaidi kwa ajili ya Watanzania.
Amesema msimu huu utakuwa wa kipekee kwani, mbali na uimbaji, wameongeza vipaji vingine vikiwemo uchezaji, uchekeshaji (comedy), uigizaji, sarakasi na uchoraji, tofauti na misimu ya awali iliyojikita zaidi kwenye uimbaji pekee. “Kwa msimu huu, mshiriki anatakiwa awe na kipaji, kujiamini, mwonekano wa kistaa na kupendeza. Baada ya kuwa na sifa hizo, ajitokeze kwenye usahili na kuonesha kipaji chake,” amesema Paulsen.

Ameongeza kuwa usahili wa vipaji vyote utafanyika kwa wakati mmoja, huku washiriki waliowahi kushiriki misimu ya nyuma bila kushinda wakihimizwa kujitokeza tena. Kuhusu usahili wa mtandaoni, amesema waombaji watapewa maelekezo maalum, kazi zao zitapitiwa na majaji, na watakaofaulu watawasiliana nao ili kufika Tanzania kuendelea na mashindano. Ameeleza kuwa kutakuwa na majaji tofauti kulingana na aina ya vipaji, na hatimaye washiriki 15 bora watachaguliwa kuingia hatua za juu za mashindano.
Kwa upande wa uzinduzi, amesema uzinduzi wa Bongo Star Search Msimu wa 16 utafanyika Nairobi Machi 12, 2026, ikiwa ni mara ya kwanza uzinduzi huo kufanyika nje ya Tanzania, baada ya uzinduzi wa awali kufanyika Dar es Salaam. SOMA: BSS 16 yazinduliwa mshindi kupata mil 50
Akizungumza kwa niaba ya Azam Media, Msimamizi wa Chanel ya Sinema Zetu, Sophia Mgaza, amesema vipindi vya Bongo Star Search vitarushwa kila Jumapili saa tatu usiku kupitia Chanel ya Sinema Zetu, huku kipindi cha kwanza kikianza rasmi Machi 22, 2026 saa mbili kamili.




Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ https://Www.Jobathome1.Com