Taifa Stars yakwamia 16 bora AFCON

MOROCCO; TIMU ya Taifa ya Tanzania βTaifa Starsβ imeshindwa kuingia robo fainali ya michuano ya Mataifa ya Afrika baada ya kufungwa bao 1-0 na wenyeji Morocco katika mchezo wa hatua ya 16 bora usiku huu wa Janauri 04, 2026.
Hata hivyo wachezaji wa Taifa Stars walimlalamikia kwa kiasi kikubwa mwamuzi Boubou TraorΓ©, wakionekana kupinga kwa kiasi kikubwa maamuzi yake ikiwemo madai ya kuwanyima penalti dakika za mwishoni za mchezo huo.

Morocco walimaliza kileleni mwa Kundi A wakiwa na pointi saba, huku Taifa Stars wakiwa nafasi ya tatu katika Kundi C ikiwa na pointi mbili, wakiibuka kati ya timu zilizoshika nafasi za washindwa watatu bora.
Taifa Stars ilifungwa na Nigeria 2-1 katika mchezo wa kwanza, kabla ya kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Uganda na Tunisia.

Morocco βSimba wa Atlasβ waliichapa Comoro mabao 2-0, sare ya 1-1 na Mali na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Zambia.
Jana Serikali ya Tanzania iliizawadia Taifa Stars kiasi cha Sh milioni 500, kufuatia kufuzu hatua ya 16 Bora katika michuano ya AF CON 2025.




