Boti ya abiria yazama ,10 wako salama

NIGERIA : ZAIDI ya watu 40 hawajulikani waliko baada ya boti ya abiria kuzama Jumapili, Agosti 17, 2025, nchini Nigeria. Idara ya huduma za dharura imesema watu 10 waliokuwa kwenye boti hiyo wameokolewa salama.

Chombo hicho kilikuwa kimebeba abiria wasiopungua 50 waliokuwa wakielekea kwenye soko maarufu la Goronyo, jimbo la Sokoto. Mkuu wa idara hiyo, Zubaida Umar, amesema kwamba wanashirikiana na mamlaka nyingine za ndani ili kuwatafuta na kuwaokoa waliopotea.

Tukio hili linajiri wiki tatu baada ya boti nyingine kuzama katika jimbo la Niger, ambapo watu 13 waliokufa maji na makumi mengine walipotea, huku abiria walikuwa wasiopungua 100. SOMA: Watu 26 wauawa kwa bomu Nigeria

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button